Wabunge wa upinzani jana walitoka nje ya ukumbi wa bunge mjini
Dodoma, wakipinga kitendo cha Naibu spika wa Bunge hilo Dk. Tulia Akson
kutotoa nafasi ya kujadiliwa kwa hoja ya haki za bunge, kama
ilivyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Mjini, Bw. Zito Kabwe.
Wakizungumza nje ukumbi wa bunge, baadhi ya wabunge hao wa upinzani, wamedai kuwa mhimili wa bunge kwa sasa umekuwa hauheshimiwi, na kwamba kanuni za bunge zimekuwa hazifuatwi, kutokana na wabunge kukamatwa ovyo na polisi, bila ya kutolewa sababu za kukamatwa kwao.
Kitendo cha wabunge hao kutoka nje ya ukumbi wa bunge kinafuatia jeshi la polisi kumkamata mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu ambapo wamedai taarifa hiyo haikutolewa bungeni wala sababu ya kukamatwa kwake.
WAWEZA SIKILIZA ZAIDI WALICHOKISEMA HALIMA MDEE, ZITTO KABWE NA WENGINE KWA KUBONYEZA PLAY HAPO CHINI

0 comments:
Post a Comment