Rapa wa kike bongo Chemical ambaye siku za karibuni aliweka wazi kuwa
mpaka sasa bado hajapoteza usichana wake amefunguka na kusema toka watu
wamesikia jambo hilo kuna watu wengi wamekuwa wakijitokeza na kutaka
kumtafutia mwanaume.
Akiongea kwenye kipindi cha eNEWZ Chemical alisema Wema Sepetu si
kweli kama alikuwa anamtafutia mwanaume bali Wema Sepetu alikutana naye
na alikuwa naye karibu sana kipindi ambacho walikuwa wanatengeneza
filamu ya 'Mary Mary' ila amekiri kuwa wapo baadhi ya watu ambao
wamekuwa wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.
"Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine
wanasema sikuwa na busara kufanya vile. Lakini nataka kuwaambia kwanza
sikujitangaza ila ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana
siwezi kuvijibu. Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa
wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo,
mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye
'Career' yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae
kuniharibia maisha yangu" alisema Chemical
Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamekuwa
wakijitokeza kutaka kumtafutia mwanaume na kusema yeye hana shida hata
wakimtafutia mwisho wa siku yeye lazima ampime kuona kama anamfaa au
hafai.
"Wema Sepetu tumekutana kwa ajili ya movie, kuna movie tulikuwa
tunashoot inaitwa 'Mary Mary' kwa hiyo kipindi kile watu walikuwa
wananiona na Wema ni kipindi ambacho muda mwingi tulikuwa location. Ila
akinitafutia kama dada means kwamba ataona kuwa huyo mwanaume ananifaaa
siyo Wema Sepetu tu wapo watu wengi wanajitokeza kumtafutia Chemical
mwanaume kwa hiyo kama wataona huyo mtu ni mtu sahihi kwangu waniletee
na mimi nitamwangalia nikiona ni mtu sahihi sawa hivyo wanajitokeza
wengi kunitafutia wanaume ila siyo Wema" alisema Chemical


0 comments:
Post a Comment