Dar es Salaam: Huku akitumia
nguvu kubwa kukanusha, sexy lady anayefanya ‘fresh’ kwenye Bongo Fleva,
Esterlina Sanga ‘Linah’ amegandwa na skendo ya kudaiwa kuvuta sigara,
sambamba na matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’,
Awali, chanzo ambacho ni rafiki wa Linah
kilidai kuwa, mwanadada huyo ambaye ni mmoja wa wasanii wa kike wenye
mafanikio kwenye muziki huo kwa sasa, amekuwa akiongozana na marafiki
ambao si wazuri na wamefikia hatua ya kumuingiza kwenye tabia zisizofaa
ikiwa ni pamoja na utumiaji wa sigara na ‘mitungi’.
“Linah ni rafiki yangu sana lakini
hakuna kitu kinachoniumiza kama kumuona anavuta sigara. Kuna mtu
alinitonya juu ya tabia yake hiyo nikawa sikuamini lakini hivi karibuni
niliona picha zake akiwa ameshika sigara anavuta bila wasiwasi.
Mbaya zaidi naambiwa eti na yeye
anatumia unga, kwa kweli yote naweza kumvumilia lakini kama kweli na
kwenye unga kaingia, atakuwa anataka kupotea, ni vyema akaangalia upya
marafiki zake.
“Zamani alikuwa rafiki mkubwa sana wa
Recho (Winfrida Josephat), yule wa THT, naye mara nikasikia anavuta
bangi, mara unga, nikasema Linah ajiangalie sana maana rafiki yako akiwa
mwizi hata wewe ni rahisi kuwa mwizi,” alisema rafiki huyo wa Linah
aliyeomba hifadhi ya jina
MWENYEWE ANENA
“Jamani hilo suala la unga wala siyo kweli, hivi sijipendi kweli? Kama
mimi natumia unga basi nife! Nawaona watu wanavyoangamia na janga hilo
halafu mimi nijiingize huko, aah! Hilo haliwezekani,
Mimi najitambua sana tena zaidi ya
sana, siwezi kujiingiza kwenye mambo ambayo najua yanaweza kuniharibia
maisha yangu. Nafanya muziki, watu wanipe sapoti kwenye hilo na
wasizushe mambo ambayo hayapo." alisema Linah.
Linah alikuwa shosti mkubwa wa Recho wa
THT ambaye aliwahi kudaiwa kujiingiza kwenye utumiaji wa unga. Mwanadada
huyo aliibuka na kukanusha madai hayo ila akakiri kuwa aliwahi kuvuta
bangi, jambo lililowashangaza wengi.
0 comments:
Post a Comment