Imetokea sintofahamu kwa wanafunzi wa special diploma (Education) baada ya kuambiwa chuo kimefungwa kwa upande wao hadi hapo watakapotangaziwa mustakabali wao.
Jana, lilitolewa tangazo chuoni hapo likiwataka wanafunzi hao kuondoka kati ya jana hadi leo saa 12 jioni. Tangazo hilo lilieleza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo katika ufundishaji wa stashahada hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imeamua wanafunzi hao kurejea majumbani na wataelezwa mustakabali wao “mapema iwezekanavyo”.
Hii ilianza pale ambapo wanafunzi hao walipoanza kudai haki yao ya kufundishwa baada ya kutoona mwalimu yeyote akiingia darasani kwa takribani wiki tatu sasa.
0 comments:
Post a Comment