Post ya kwanza ya ROMA tangu alipotekwa…ni simulizi ya kweli? - ABETIGER UPDATES <script async='async' src='//pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js'></script> <!-- Adslinks --> <ins class='adsbygoogle' data-ad-client='ca-pub-9050840540045431' data-ad-format='auto' data-ad-slot='2619472872' style='display:block'></ins> <script> (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); </script>

Post ya kwanza ya ROMA tangu alipotekwa…ni simulizi ya kweli?

Zaidi ya miezi mitatu imepita tangu mara ya mwisho rapa Roma Mkatoliki kupost kwenye Instagram ambapo baadaye alitoa ahadi ya kufanya hivyo kama video ya wimbo wake mpya ‘Zimbabwe’ aliyoitoa karibuni ingefikisha Viewers Milioni Moja.

Sasa good news ni kwamba , leo August 24, 2017 Roma Mkatoliki ameweka post ya kwanza kwenye Instagram yake na kitu alichokipost ni hiki hapa.

#Sehemu_Ya_1
Ilikuwa Ni Usiku Majira Ya Saa Saba Kasoro, hali ya hewa ikiwa ni ya ubaridi kutokana na Mvua zilizokuwa zinanyesha Kipindi hicho, zilizoambatana na upepo mkali uliokuwa unavuma pembezoni mwa Bahari,
Ilisikika Sauti Ya Mtoto Mchanga akilia saanaa Katika Moja Ya wodi ya Hospitali fulani Iliyokuwa Imejengwa Pembezoni mwa Bahari Hiyo.Nilihadithiwa kuwa ilikuwa ni siku ya Ijumaa Ya Tarehe 12 mwezi wa 12 miaka ya 80 naa(Takribani Miaka zaidi ya 30 sasa imepita), Katika Hospitali Ya Bombo Mkoani Tanga (Mjini), sauti hiyo ya kichanga kilichokuwa kinalia ilikuwa ni ishara kuwa ulimwengu umeongeza kiumbe mwingine katika Ardhi Ya Tanzania Barani Afrika.
Alionekana Mwanamke Amejilaza kitandani akiwa amechoka huku pembeni yake kikiwepo kichanga hicho chenye Kg 3.5 Na afya Njema Bila Kasoro yoyote, Kikinyonya Ziwa la kuume la mama huyo, hakika ilikuwa ni furaha kwa familia hii.
Furaha iliongezeka zaidi pale ilipofika muda wa kuona wagonjwa ambapo familia yote akiwemo baba wa kichanga hiki alikuja kumuona kidume wake, na jambo lililofurahisha zaidi ni kuwa kila mtu katika familia (kaka/dada/mamdogo) alikuwa ana jina lake kichwani alilopanga kumpatia kichanga hiki,
wakati huo huo mama mzazi yeye alishapanga jina lake la kumpa mwanae, Ndipo mabishano yalipoanza wodini hapo kila mtu akisema aitwe flani aitwe flani aitwe flani….kelele hizo zilipelekea Nurse wa zamu awatoe Nje Kwa sababu ilikuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wengine,
ikawa hivyo siku ikaisha kichanga hicho hakijapatiwa jina.Baada ya muda mama na mwanae walipata ruhusa kurudi nyumbani na ukawa mwanzo wa maisha mapya katika familia hii.Lakini Siku tu mama huyu alipokifukia tu kitovu cha mwanae na kumpa jina #Ibrahimhuku baba mtu akikataa na akitaka mtoto aitwe #Ismail au #Isihaka na ndugu wengine walitaka mtoto aitwe #Idrissandipo visa/mikasa/misukosuko ilipoanza kuiandama familia hii…..

#ITAENDELEA………. Click Link on My Bio.
#A_Journey_To_Zimbabwe

About Tiger

Tiger
Recommended Posts × +

0 comments:

Post a Comment