Utatu wa BBC ulivuma sana lakini sasa Bale ana majeruhi kila
siku,Benzema hayupo katika fomu kubwa na utatu wao sio tishio kama
zamani lakini hawa wafuatao ndio (trio) utatu bora zaidi kwa
waluchofanya msimu huu.
10.Mkhitaryan,Ibrahimovich & Mata.
Pamoja na kuwa katika nafasi ya sita lakini ni jambo
lililo dhahiri kwamba United wako katika kiwango kizuri sana kwa
sasa.Lakini tangu December 4 baada ya Mkhtaryan kuanzishwa katika kikosi
cha kwanza cha United wamekuwa na safu yenye unyumbulikaji,toka
muunganiko huu uanze kuchezeshwa katika mechi 10 za mwanzo kuanzia
December 4 United walishinda mechi 6 na kusuluhu 4.Combination hii
imefunga magoli 25 jumla kati ya magolu 40 ya United huku Zlatan
akifunga 16.
9.COUTINHO,FIRMINHO & MANE.
Huu ni utatu ambao umeshindwa kucheza pamoja kwa muda
mrefu kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo pamoja na majeruhi na Mane
alirudi nyumbani kwa ajili ya Afcon.Ila hii haijawazuia kufunga magoli
24 kwa pamoja hadi sasa.
8.PERROTI,DZEKO NA SALAH.
Dzeko ni kati ya washambuliaji tishio sana kwa wapinzani
kwa sasa lakini combinationa yake na Perroti na Salah inawafanya kwa
pamoja kuwa tishio sana.Salah ni mchezaji wa pili kw key pass Italia
akipiga pasi 45 Perroti ameleta balaa kubwa upande wa kushoto na hawa
wawili kwa pamoja wana magoli 14 huku Dzeko akiweka 18 kambani na
kuifanya Roma kuwa nafasi ya pili Serie A.
7.RIBERY,LEWANDOSKI NA ROBBEN.
Robben na Lewandoski walishiriki kuiadhiri Arsenal pale
Allianz Arena.Baada ya Muller kutokuwa na msimu mzuri huku Douglas Costa
naye akiwa haeleweki msimu huu.Kwa msaada wa kiungo Thiago Alcantara
unawafanya Lewandoski,Robben na Ribery kuwa hatari na kuifanya Bayern
Munich kuongoza ligi ya Ujerumani na pia kuwa tishio barani Ulaya.
6.SANE,JESUS NA STERLING.
Utatu mpya ambao umeingia doa baada ya Jesus
kuumia.Tangu kuwasili kwa Jesus utatu huu umekuwa tishio sana na
kumfanya mshambuliaji hatari Kun Aguero kuanza kusugua benchi.Kabla ya
kuumia Jesus alishafunga magoli matatu katika mechi mbili,Strling nae
anaonekana kuimarika huku pembeni Sane akionekana kuanza kuwasha moto.
5.DEMBELE,AUBEMAYANG NA PULISIC.
Dortmund hawako katika msimu mzuri sana lajini hadi sasa
Piere Aubemayang tayari ameshafunga magoli 17.Dembele amekuwa gumzo
msimu huu akitajwa kuwa ni kati ya wachezaji vijana wa kuchungwa na
muunganiko wake na Pulisic unaonekana muunganiko wa vijana wadogo lakini
hataru hadi sasa wana assist nane na magoli manne.
Di Maria aliwafunga Barcelona goli 2,Cavani 1,Draxler 1
wakaiua Barcelona 4.Cavani msimu huu ni tishio kubwa katika mechi 29
alizoamza amefunga magoli 32.Ujio wa Draxler Psg umewafanya warudishe
kitu katika timu yao baada ya Ibrahimovich kujiunga United,Draxler
amefanikiwa kuifanya safu ya ushambuliaji ya PSG kuonekana tishio tena.
3.HAZARD,COSTA NA PEDRO.
Imekuwa kawaida kwa hawa watatu kufunga kila wiki,wiki
iliopita Pedro na Costa waliipeleka Chelsea robo fainali ya FA.Mfumo wa
3-4-3 wa Antonio Conte umefanya hadi sasa kwa pamoja kufunga mabao 31 ya
ligi,lakini vilevile kwa pamoja Pedro,Costa na Hazard wana assist 13 na
wameusogeza timu yao karibu kabisa na ubingwa.
Hakuna beki anayetamani kuwakabili MSN ni hatari kubwa
sana.Messi ana jumla ya magoli 26,Suarez ana 20 huku Neymar akiwa ana
assist 14.Kwa misimu miwili MSN imekuwa gumzo sana kutokana na uwezo wao
mkubwa,ushirikiano na jinsi ambavyo wanatengeneza nafasi,huwezi
kuwaacha ukitaja washambuliaji hatari mno kwa sasa.
Unaweza kushtuka,haswa kama sio mfuatiliaji wa ligu zote
5 kubwa barani Ulaya lakini amini Napoli wana huu utatu ambao unavutia
kuliko hizo tatu zote ulizoziona hapo juu.Mertens ana miaka 29 na
Callejon ana 30 lakini kwao umri suo tatizo hata kidogo kwani katika
mechi 11 zilizopita wana hattrick 2 na kufunga jumla ya magoli
14.Callejon amekuwa mbunifu sana kwani ana assist 9 hadi sasa na uwepo
wa Insignes nyuma yao kuwafanya kuonekana hatari,haitakuwa jambo la
ajabu kwa Napoli kupindua matokeo ya mchezo wao wa kwanza waliofungwa
goli 3 kwa 1 na Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment