RAYVANNY KUFANYA KOLABO NA ALLY KIBA? - ABETIGER UPDATES <script async='async' src='//pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js'></script> <!-- Adslinks --> <ins class='adsbygoogle' data-ad-client='ca-pub-9050840540045431' data-ad-format='auto' data-ad-slot='2619472872' style='display:block'></ins> <script> (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); </script>

RAYVANNY KUFANYA KOLABO NA ALLY KIBA?

Ushindani kwenye Muziki wa kizazi kipya umekuwa mkubwa hasa kwa wasanii nguli wa muziki huo Diamond Platnumz na Ally Kiba.Ushindani ambao umepelekea kuibuka kwa upinzani mkubwa baina ya wasanii hao kiasi cha watu kudhani kuwa imeathiri uhusiano baina ya watu wa karibu wa wasanii hao.
Msanii wa muziki kutoka label ya WCB, Rayvanny amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na Alikiba ambaye ni mpinzani mkubwa wa boss wake Diamond Platnumz.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na single aliyoshirikishwa na QueenDarling, KIJUSO, amedai yeye hana tatizo na Alikiba na hata ikitokea nafasi ya kolabo atafanya naye.
“Alikiba huwa nikikutana naye huwa napiga naye stori, tunasalimiana tunacheka, ananiambia kuwa nafanya kazi nzuri, hatujawahi kuongea sana,” Rayvanny alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
Aliongeza,”Ikitokea siku naweza kufanya naye kolabo kwasababu ‘end of the day’ wote tunafanya muziki ni biashara pia, mashabiki wetu wanapenda kuona ‘combination’ za watu tofauti tofauti, hata nikikutana naye hatufungiani vioo,”
Diamond na Alikiba wana ushindani mkubwa kiasi cha kuonekana wana bifu zito linalochochewa hasa na mashabaki wa wasanii hao nguli wa Bongofleva, hususan kwenye mitandao ya kijami.

About Tiger

Tiger
Recommended Posts × +

0 comments:

Post a Comment