IDADI YA KURA ALIZOPATA SAMATTA. - ABETIGER UPDATES <script async='async' src='//pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js'></script> <!-- Adslinks --> <ins class='adsbygoogle' data-ad-client='ca-pub-9050840540045431' data-ad-format='auto' data-ad-slot='2619472872' style='display:block'></ins> <script> (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); </script>

IDADI YA KURA ALIZOPATA SAMATTA.



Mbwana Samatta ndio jina liliotajwa zaidi kwenye vinywa vya watanzania wengi na Afrika kiujumla ndani ya masaa kadhaa yaliyopita – baada ya mwanasoka huyo wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Anayecheza Ligi za Ndani ya Afrika.
Ushindi wa Samatta, ambaye ni mshindi wa na mfungaji bora wa ligi ya mabingwa wa Afrika umetokana na kuwashinda wapinzani wake Zein Edin Farahat, Roger Assale, Robert Kidiaba, Moudather el Tahir,Mohammed Meftah, Kermit Erasmus, Felipe Ovono, Baghdad Bournedjah, na Abdeladim Khadrouf.
Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Utaratibu wa CAF – Shirikisho la soka katika upigaji kura wa kumchagua mshindi wa tuzo hii unatokana na kura zilizopigwa na makocha wa timu za taifa au wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vya nchi za kiafrika.
Kwa mwaka huu wachezaji wote hao waliotajwa hapo juu walipigiwa kura na matokeo kwa walioingia tatu bora ni kama yanavyoonekana kwenye mpangilio hapo chini.
Mbwana Samatta - 127
Robert Kidiaba - 88
Baghdad Bournedjah - 63 

About Tiger

Tiger
Recommended Posts × +

0 comments:

Post a Comment